Pichani ni mmoja kati ya waandamanaji hao aliyekuwa karibu na Dkt Kigwangala akiwa chini baada ya kujeruhiwa na polisi |
Mlipuko wa mabomu kwa mbali |
Awali mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kigwangala akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini hao katika kijiji cha Nzega Ndogo kabla ya maandamano |
Maandamano baada ya mkutano wa Dkt Kigwangala kuelekea eneo la machimbo ya Mwashina wilayani NZega. |
Jeshi
la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora jana limemkamata mbunge wa
jimbo la Nzega Dkt. Hamis Kigwangalla aliyekuwa kwenye maandamano ya
wachimbaji wadogo wa dhahabu ya kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya
Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited.
Kabla
ya hapo mbunge huyo alifanya mkutano mkubwa wa hadhara na wachimbaji
hao katika kijiji cha Nzega Ndogo wilayani humo ambapo alielezwa
matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na kamishna wa madini nchini Bw.
Paulo masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao wadogo
kwenye eneo hilo.
Katika
mkutano huo wachimbaji hao walidai ni vema serikali iangalie haki zao
zilizotumika kwenye uendeshaji na uchimbaji wa mashimo hayo kuliko
kuwafungia bila kujali ingawa eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa
Resolute lakini wao ndiyo wamiliki wa ardhi hiyo.
Hata
hivyo katika hoja hiyo mbunge huyo aliwataka wachimbaji hao kudai haki
yao kwa kufuata taratibu zinazostahili bila kujali tofauti zao kisiasa,
kikabila na kidini na badala yake wawe kitu kimoja.
Baada
ya kauli hiyo mbunge huyo aliwaambia wachimbaji hao wadogo kuwa haki
yao iko mikononi mwao hivyo ni uamuzi wao wa kudai haki yao na yeye kama
mwakilishi wao yuko nyuma yao mpaka pale haki yao itakapopatikana.
Wachimbaji
hao walimwomba mbunge huyo kuambatana nao kwenye maandamano ya amani
kutoka kijiji cha Nzega Ndogo kwenda Mwashina yalipo machimbo
yaliyofukiwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu kujionea hali halisi ya
kufukiwa kwa eneo hilo na ikiwezekana kufanya mkutano mwingine wa
hadhara kijijini hapo.
Kufuata
hali hiyo wachimbaji hao walianza maandamano ambayo yaliungwa mkono na
mbunge huyo hadi kijiji cha Mkwajuni kabla ya kufika Mwashina ambapo
polisi waliibuka na kuyasambaratisha maandamano hayo kwa mabomu ya
machozi na risasi za moto.
Katika
na purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na
kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo
waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.
Awali
askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari
kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali na matumisi ingawa hali hiyo
ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.
Kamanda
wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda alipopigiwa simu na waandishi wa
habari alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na maandamano hayo,
kukamatwa kwa mbunge huyo wa jimbo la Nzega na kutumika kwa risasi za
moto na mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo.
Tayari Dkt Kigwangala ametoka polisi usiku wa kumkia leo
Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora.Credit Jiachie Blog
Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora.Credit Jiachie Blog
Post a Comment