Kaimu
Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi akitoa taarifa kwa
Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhusu hali ya upatikanaji wa maji kwenye
halmashauri hiyo wakati wakiwa kwenye moja ya kisima kinachotumika
kusukuma maji kupeleka kwenye tanki la maji kasha kusambazwa katika
maeneo mengine kijijini hapo
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali Ngemela Lubinga ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Mlele wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa tenki la
maji lenye uwezo wa kuhifadhiwa lita 90,000 za maji na litaweza
kuhudumia wakazi wapatao 2000 katika kijiji hicho cha Isinde siku ya
kilele cha wiki ya maji .viongozi wa mkoa huo.
Na Kibada Kibada Katavi
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewahimiza wananchi wa Mkoa huo
kutunza mazingira na kutoharibu vyanzo vya maji kwani kutofanya hivyo
kunaleta madhara makubwa katika maisha ya kila siku.
Akiongea
na wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele
cha maji Mkoa yaliyofanyika kwenye kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda,
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu amesema wananchi wanatakiwa kutunza mazingira
na kuhifadhi vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu.
Katika
hotuba yake hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya huyo,
imeeleza changamoto hizo za uharibifu wa mazingirazi
zinazoukabili Mkoa wa Katavi kuwa ni uhamiaji holela wa wananchi kutoka
mikoa ya Kigoma, Mwanza,Tabora,Simiyu na Shinyanga ambapo humami a na
kuchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu kwenye vyanzo vya maji na
mazingira
Aidha
amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili kutunza na kuendeleza miradi
ya maji waliyojengewa na serikali ili iweze kuwanufaisha wananchi wa
Mkoa huo kwa kuwaondolea matatizo ya upungufu wa maji uliokuwa
ukiwakabili.
Katika
hatua nyingine amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili fedha
inayopatikana isaidie kuendeleza ukarabati unaoweza kijitokeza iwapo
kutakuwa na uharibifu wowote kwenye mradi wa maji kwa kuwa miradi ya
maji ni mali yao.
Awali
Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi katika
taarifa yake ya ujenzi wa tanki la maji alieleza kuwa zaidi ya shilingi
milioni 200 zimetumika katika ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo
wa kuchukua ujazo wa lita 90,000 (90m).
Msengi
ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuwaondolea kero ya
maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha Isinde kwa muda
mrefu.
Naye
Mhandisi wa Maji Mkoa wa Katavi, Elieda Mwakasungura katika Taarifa
yake ya Mkoa wa kuhusu maji alieleza kuwa wananchi wanaopata maji safi
na salama katika mkoan huo ni asilimia 48 hali ambayo inaonesha bado
lipo tatizo la upatikaji wa maji safi na salama katika mkoa huo.
Miradi
mingine inaendelea kutekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda
katika kijiji cha Ikola,Ngomalusambo na Karema,miradi mingine
inatekelezwa katika Halmashauri ya Nsimbo.
Post a Comment