Watu wawili wamefariki dunia kwa kuangukiwa na nguzo za umeme Butiama.
Watu wawili
wamefariki dunia papo hapo na wengine kumi na mmoja kujeruhiwa vibaya
wakati wakifanya kibarua cha kushusha nguzo za kusambazia nishati ya
umeme vijijini kupitia kampuni ya moja ya Derm katika kijijini cha
Bisumwa wilayani Butiama mkoani Mara.
Baadhi ya
majeruhi wa ajali hiyo wamesema tukio hilo limeokea leo saa 3.30
asubuhi katika kijiji cha Bisumwa wilayani Butiama,ambapo vibarua hao
kutoka kijiji cha sabasaba baada ya kufika kijijini hapo na lori hilo
aina ya Scania yenye namba za usajili T 787 CUL wakiwa juu ya sheena
hiyo ya nguzo na wakati wajaribu kufungua mikanda kwa ajili ya
kuzishusha nguzo hizo zilishuka kwa kasi kubwa sambamba na wao hatua
ambayo imesababisha watu wawili kufariki dunia kwa kugongwa na nguzo
hizo huku wengine wakipata majeraha makubwa yakiwemo ya kuvunjika kwa
miguu.
Viongozi
wa halmashauri ya Butiama wakiongozwa na mwenyekiti wake Bw Magina
Magesa, ambao walifika muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea kwa ajili
ya kutoa msaada kwa majeruhi hao,pamoja na kutoa pole lakini wametaka
kampuni zinazohusika kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vya mkoa
wa Mara kuchukua tahadhari wakati wa kusafirisha nguzo hizo ili kuepuka
ajali mbaya kama hiyo.
Kaimu
kamanda wa polisi wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa jeshi la
polisi Paul Kasabago, akizungumza na ITV kwa njia ya simu amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu kuwa ni Masui Magibo (20) na
Salabanze John (22) wote wakazi wa kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama
na kwamba majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara
mjini Musoma kwa ajili ya matibabu zaidi.
Post a Comment