VIONGOZI
wa serikali mkoa wa Dodoma wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Rehema
Nchimbi wakiwa wamejipanga tayari kumpokea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
wakati wa kutembelea mradi wa visima virefu vya maji eneo la Kibaigwa,
wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma.
Mradi huo wa maji una thamani ya zaidi ya shilling billion 2.3.
Ufunguzi
wa mradi huo ni sehemu ya maadhimisho ya 26 ya Wiki ya Maji ambapo
kitaifa yanafanyika Dodoma tarehe 16-22/03/2014. Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk Jakaya Kikwete.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk Rehema
Nchimbi mara baada ya kuwasili eneo la mradi wa visima vya maji,
Kibaigwa.
Injinia
Emmanuel Mwakabole kutoka Mamlaka ya Maji Dodoma (DUWASA) akitoa
maelezo ya mradi kwa waziri mkuu na kusema visima viwili vyenye kina cha
meta 105 vina uwezo wa kuzalisha maji lita 90,000 kwa saa. Muonekano wa jengo lenye genereta ya akiba ya kuzalisha umeme endapo umeme wa gridi unakatika
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DODOMA
Post a Comment