Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa katika zoezi la
ukaguzi wa mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu na
huduma za mama wajawazito na watoto wachanga katika maadhimisho ya siku
ya Utepe Mweupe Tanzania yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa katika
Tarafa ya Mtowisa. Dkt. Seif Rashid alimuwakilisha Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambae
awali alikubali kushiriki maadhimisho hayo ambapo amekabiliwa na
majukumu mengine ya kitaifa. Kushoto kwa Dkt. Seif Rashid ni Mratibu wa
Taifa wa Utepe mweupe Mama Rose Mlay. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo
ikiwa ni “WAJIBIKA MAMA AISHI”
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akihutubia katika
maadhimisho hayo ambapo aliwapongeza wadau wote wanaopigania na kusaidia
afya ya mama na watoto na kuahidi kutoa kipaombele katika bajeti kwa
ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto nchini.
Aidha amezitaka Halmashauri nchini kutoa kipaombele kwa kuongeza bajeti
zao katika kuhudumia afya ya mama wajawazito na watoto wachanga.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa salamu za Mkoa wa
Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya katika
Maadhimisho hayo ya kitaifa. Katika Salamu hizo alisema zipo changamoto
nyingi katika sekta ya afya zinazohitaji ufumbuzi wa haraka ikiwemo
upungufu wa watoa huduma, vifaa tiba, dawa, magari ya kubebea wagonjwa,
vituo vya kutolea huduma za afya na vingine kuwa mbali na maeneo ya
wananchi kwa baadhi ya maeneo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akifafanua baadhi ya mambo katika sekta ya afya Mkoani Rukwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akikabidhi kwa Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii Dkt. Seif Rashid maoni na maombi ya wakazi wa Wilaya yake
katika kuimarisha sekta ya afya katika Wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
Maadhimisho
hayo yalitawaliwa na hali ya hewa ya mvua ambayo hata hivyo haikuathiri
mwenendo mzima wa ratiba iliyopangwa, baadhi ya wananchi walilazimika
kutumia miamvuli na wengine kuonyesha uzalendo mkubwa na kuamua
kunyeshewa hadi kukamilisha maadhimisho hayo, hata hivyo mvua hiyo
ilikatika karibu na kufikia mwishoni mwa maadhimisho hayo.
Bi
Adrianne Strong ambae nae ni mdau wa afya ya mama wajawazito na watoto
wachanga akitoa salam zake na kujitambulisha. Hivi karibuni Bi Adriane
Stong kwa
kushirikiana na waumini wenzake wa Kanisa la University United
Methodist Church la Washington DC Marekani walitoa msaada wa boti na
life jacket kwa ajili ya kusaidia huduma za afya ya mama wajawazito na wagonjwa mwambao wa Ziwa Rukwa.
Balozi
wa Utepe Mweupe Tanzania ambae pia ni mwanamuziki Sara Thomas
akijumuika na wanawake wengine kuimba wimbo wa kuihimiza Serikali na
wananchi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanaokoa maisha ya mama
wajawazito na watoto wachanga.
Zoezi
la uchangiaji wa damu salama lilikua likifanyika katika kila Wilaya za
Mkoa wa Rukwa katika wiki ya maadhimisho hayo ya utepe mweupe ambapo
chupa za damu zaidi ya alfu moja zilichangiwa na wananchi wa Mkoa wa
Rukwa.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
Post a Comment