CP
Mussa Ali Mussa, akitoa maagizo kwa Wakaguzi wa Polisi wanaoshiriki
katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya kudhibiti rushwa
yanayofanyika mjini Dodoma.
Wakaguzi
wa Polisi kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaoshiriki mafunzo ya
miundombinu ya maadili na mikakati ya kupambana na vitendo vya rushwa
wakimsikiliza Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP. Mussa Ali Mussa,
wakati akitoa mada juu ya umuhim wa Polisi Jamii.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
katikati akiwaelekeza jambo waandishi wa Habari wa Jeshi la Polisi
walioshiriki katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya
kupambana na rushwa. kushoto ni Insp. Dickison Gibeshi na kulia ni Sgt
Shabani Msangi,
………………………………………………………………………………..
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Dodoma
DODOMA, JUMAPILI MACHI 16, 2014.
Maafisa na Askari Polisi hapa nchini, wametakiwa badili tabia zao kwa
kujiepusha na vitendo vya kudai na kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye
Matatizo yanayohitaji huduma za kipolisi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo
Ufuatiliaji na Tathimini cha Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna
(DCP) Mpinga Gyumi, wakati akitoa mada kwa washiriki wa Mafunzo ya
kuimarisha Miundombinu ya Maadili na mapambano dhidi ya Rushwa
yanayotolewa kwa Wakuu wa Polisi wa Tarafa na Majimbo yanayofanyika
mjini Dodoma.
DCP Gyumi, ameonya kuwa Jeshi la
Polisi halitamvumilia Afisa ama Askari yeyotw atakayekwenda kinyume na
maadili ya Jeshi hilo jambo ambalo amesema limekuwa likipakwa matope.
Akikariri baadhi ya vifungu
vilivyomo kwenye kitabu cha miongozo ya Jeshi la Polisi nchini Police
General Order (PGO), amesema kitabu hicho kimetoa makatazo kwa Askari
Polisi wa vyeo mbalimbali na kutoa maelekezo mazuri yanayofaa kufuatwa
na kila Askari Polisi.
DCP Gyumi pia amewakumbusha
Maispekta hao pamoja na Maafisa wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo kujiepusha
na vitendo vya kupokea zawadi kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na
kuhalalisha rushwa.
Amesema rushwa imekua ikipunguza
heshma na uadilifu kwa mtumishi na hivyo kumfanya kushindwa kuheshimu
sheria, kanuni, taratibu na kuwafanya baadhi ya watumishi kujilimbikizia
mali kwa njia zisizo halali, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma.
Amewaonya wale wote wanaojihusisha
na matumizi mabaya ya mali za umma kama vile magari, kompyuta, mashine
na vitendeakazi vingine kuacha kufanya hivyo kwani matokeo yake ni
kuitia serikali hasara.
Amewataka Maafisa na Askari wa
ngazi zote kuwa wasafi mbele ya Jamii hali itakayilifanya Jeshi la
Polisi kuwa kimbilio la wanyonge na sio kukimbiwa. “ Nawaombeni kila
mmoja wenu kutimiza wajibu wake na kuzaliwa upya hata kama anadhani
ameshindikana”. Alisema DCP Byatao.
Naye Kamishna wa Polisi Jamii
nchini CP Mussa Ali Mussa, amewataka Mainspekta hao kuhakikisha kuwa
wanaondokana na vitendo vya kudai na kupokea rushwa ili wawe mfano bora
kwa jamii na Askari waliochini yao.
Awali Mkuu wa Kitengo cha Maadili
na Nidhamu cha Jeshi la Polisi nchini SACP Patrick Byatao, alisema hadi
sasa, zaidi ya Polisi 1,100 wakiwemo Maafisa Wanadhimu wa Polisi wa
mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa wilaya na wa Usalama Barabarani hapa
nchini, wameshanufaika na mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Shirika la
Misaada la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID).
Post a Comment