Waziri
wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe (katikati), akikata utepe kuzindua
rasmi maadhimisho ya 26 ya wiki ya maji yanayofanyika kitaifa katika
uwanja wa jamuhuri Mkoani Dodoma Machi 16-22,2014 (kushoto), Katibu Mkuu wa wizara hiyo Enjinia Bashir Mrindoko, na kulia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, kuhusiana na maendeleo ya miundo mbinu ya maji kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Waziri
wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe akisoma hotuba yake Machi 16, 2014
wakati akizindua rasmi maadhimisho ya 26 ya wiki ya maji yanayofanyika
kitaifa katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma,mara baada ya kufanya
uzinduzi huo Waziri Maghembe, amewataka wananchi
kuacha kutumia kuni na mkaa kwa matumizi ya nyumbani na badala yake
kutumia gesi kama nishati mbadala Maadhimisho hayo yanayolenga
kuelimisha jamii juu ya matumizi bora ya maji na mazingira , huku kauli
mbiu ikiwa ni Uhakika wa Maji na Nishart.
Baadhi ya viongozi wa serikali pamoja wananchi wakishuhudia uzinduzi huo.
Kikundi
cha ngoma cha asili ya Kigogo kikitoa burudani kwenye maadhimisho ya 26
ya wiki ya maji yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Kikundi cha ngoma cha JKT kikitoa burudani.
Mhandisi Uendeshaji kutoka DUASA, Luchanganya Nkonogumo akimuelezea Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe kuhusiana na kifaa cha kisasa kwajili ya kipimia mifereji ya maji.
Mhandisi
Mkuu Wizara ya Maji, Mwanaidi Muyimondi akimunyesha Waziri wa Maji
Profesa.Jumanne Maghembe takwimu wa ufatiliaji wa maji vijijini.baada ya
kutembelea banda la Wizara ya Maji.
Meneja
Masoko wa Kapuni ya Pipes Industries Ezra Chiwelesa akimuelezea Waziri
wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe kuhusiana pampu za kusafirishia maji
pamoja na ufanyaji kazi wake.
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akisalimiana na wanafunzi wa shule mbalimbali mara baada ya kuzinua maadhimisho hao.
Post a Comment