Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiongea
na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) na kuwaasa kutumia kalamu
vizuri hasa katika kipindi hiki cha uandaaji wa katiba mpya kwa maslahi
ya Taifa, kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO)
kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge
maalum, Leo Mjini Dodoma.
…………………………………………………
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waandishi
wa habari nchini wametakiwa kuwa wazalendo , kuzingatia maadili na
weledi wa taalum yao wakati wote watakapokuwa wanaripoti habari za Bunge
Maalum la Katiba ili kuwasaidia wajumbe kutoa mchango utakaolinda tunu
za taifa.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo
Dkt. Fenella Mukangara wakati akifungua semina ya waandishi wa habari
juu ya wajibu wao katika kuandika habari za Bunge hilo linaloendelea
mjini Dodoma.
Alisema
kuwa ni vema habari zinazoandikwa katika vyombo vya habari mbalimbali
hapa nchini wakaripoti habari ambazo zinasaidia kuimarisha na kujenga
misingi ya umoja , mshikamano , upendo na amani ,uwajibikaji na kulinda
muungano wa Tanzania.
“Tupo
hapa tulipo ndani ya muungano wetu- Nchi moja na Serikali mbili .
Tusijitume wala tusitumike na kuwajibika kubomoa jamii yetu; kwa kubeba
masuala yasiyojengeka na kuyafanya ndio ya wananchi wanayahitaji kuyajua
na tukaacha yale ya kutuwezesha kuhimiza kuipata Katiba mpya na
kusimamia wananchi kusonga mbele na kujenga nchi yetu kwa pamoja na
utulivu,”alisema Dkt. Mukangara.
Naye
Mwanasiasa Mkongwe ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
Kingunge Ngombare Mwiru, amesema mchakato wa kupatikana kwa Katiba
lazima ufanikishe kupatikana kwa Katiba iliyo bora, kama haiwezekani,
hakuna haja ya kuendelea kupoteza fedha za wananchi.
Alisema kuwa ili katiba iwe bora, lazima iboreshe muungano na umoja wa kitaifa baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kingunge
aliongeza kuwa lengo la kuundwa kwa Katiba Mpya, ni kuondoa kero
mbalimbali zilizopo hivi sasa, ziwekwe kisheria zaidi na zisimamiwe na
sheria mama ambayo ni Katiba.
Mwanasiasa
huyo mkongwe, alisema lengo la pili la kuundwa kwa Katiba mpya,
iwaletee wananchi mambo mapya ambayo yatawafaidisha wananchi.
Hata
hivyo, alisema Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa bungeni wiki
iliyopita na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba, haijachambua kwa kina kero za wananchi zinazotakiwa kufanyiwa
kazi.
Alisema imeegemea zaidi katika mustakabali wa upatikanaji wa vyeo na kuigawa nchi katika makundi ya serikali.
Kigunge
alisema licha ya mafanikio ambayo nchi imeyapata toka ipate uhuru, bado
iko nyuma kimaendeleo, kwa kuwa ina serikali ambayo ni tegemezi.
Alitolea
mfano wa wajumbe wanaozungumzia mgawanyo sawa wa madaraka uwekwe kwenye
katiba na kuacha kero msingi zinazowakumba wanawake ikiwemo ya
ukeketaji.
Kwa
upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bashiru Ali alisema
kuwa muundo wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu ya Katiba Mpya
unaiacha Serikali ya Shirikisho haina rasilimali ikwemo ardhi na
kuifanya ibaki inaelea hewani.
Alisema
kwa mujibu wa mapendekezo yaliyomo katika rasimu hiyo hakuna eneo
linaloonyesha vyanzo vya mapato ya Serikali na Shirikisho wakati
linamiliki majeshi jambo ambalo linaloweza kusababisha machafuko.
Post a Comment