Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WIZARA YA BISHARA ZANZIBAR YAPATA MSAADA KUTOKA WIZARA YA BIASHARA (SMT)

 


1
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Vifaa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael katika hafla iliyofanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar DSC_0803
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael kulia akitoa neno la Shukran baada ya Makabidhiano ya Gari na Vifaa kwa Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula. DSC_0815
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Funguo ya Gari Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael,kushoto ni Elizabeth Lukaza Mchambuzi wa Shirika la UNDP Tanzania.Hafla imefanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)

……………………………………………………………………………………
Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Wizara ya Biashara na Viwanda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Gari na Vifaa vya Ofisini kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Wizarani Malindi mjini Unguja.
Msaada huo uliofadhiliwa na Shirika la Biashara la Dunia WTO ulitolewa ili kuijengea uwezo Wizara ya Biashara ya Zanzibar katika kukabiliana na majukumu yake ya kila siku.
Akikabidhi Msaada huo Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Bara Edward Sungula kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael amesema Suala la Biashara ya Kimataifa ni la Muungano hivyo Serikali mbili lazima zishirikiane na kusaidiana katika kutekeleza majukumu yao.
Amesema Msaada huo ni utekelezaji wa Mradi wa “Capacity Building for Trade Development and Integration Project” ambao una lengo la kuzijengea uwezo Serikali katika kutekeleza misaada chini ya utaratibu wa “AID FOR TRADE”.
 Ameongeza kuwa msaada huo ni mwanzo wa kudumisha ushirikiano katika kutekeleza mradi huo na njia ya kuendeleza kudumisha Muungano uliopo baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael ameishukuru Wizara hiyo juu ya Msaada huo na kuongeza kuwa utachochea ufanisi katika majukumu yao.
Katika kutekeleza Mradi huo wa kukuza Sekta ya Biashara Tanzania Bara na Zanzibar Mradi umeanza kwa kununua Vifaa ambavyo ni pamoja na Gari mbili, Komputa, Projekta na Mashine ya Kuprintia.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top