Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigambonio Bw. Lin Tao kutoka kampuni yaChina Railway Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) akionesha
jinsi ambavyo daraja la kigamboni litakavyoonekana baada ya kukamilika.
Kulia kwake ni Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Miundombini Bw.
Hussein Mativila. Daraja hilo kutoka Kurasini mpaka Kigamboni takribani
kilometa moja litakuwa na njia sita kwa ajili ya magari. Daraja hili
linajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka
kwa Bw Lin Tao (katikati) kulia kwake (mwenye tai nyekundu) ni Naibu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za
Uzalishaji. Wa kwanza kulia (mwenye suti nyeusi) ni Meneja wa Mradi
kutoka NSSF, Bw Karimu Mataka
Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo
Picha zote na Joyce Mkinga,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Post a Comment