Wachezaji
wa Yanga wakimpongeza Nahodha wao Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya
kuifungia timu yake bao pekee katika mchezo wa leo dhidi yao na Al-Ahly
ya Misri uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam. Canavaro amefunga bao hilo kufuatia mpira wa Kona iliyopigwa na
Simon Msuva katika dakika ya 82.
Hongera Nahodha wetu.......
Hili ndilo bao la Canavaro, Kipa wa Al-Ahly akiwa hoi chini baada ya kuchambuliwa......
Kipa wa Al-Ahly akitafakari baada ya kufungwa bao hilo.....
Uwanja ulijaa kama hivi......
Mashabiki
wa Simba waliokuwa wakiishangilia timu ya Al-Ahly wakiendelea na zoezi
la kung'oa viti kama kawaida yao
Mashabiki wa Al-Ahly wakiduwaa baada ya timu yao kufungwa....
Kwa
mara ya kwanza leo mashabiki wa Yanga na wa Simba wataka kujaribu
kuchanganyikana na hii ni kutokana na mashabiki wa Yanga kuwa wengi
zaidi uwanjani, jambo ambalo lilizua mtafaruku baina ya mashabiki hao
kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki wa Simba waliokuwa
wakiishangilia Al-Ahly walianza kung'oa viti na kuwarushia wa Yanga.
Mashabiki Orignal wa Al-Ahly wakishangilia timu yao kwa nguvu zote huku wakiwasha mafataki uwanjani hapo.
Ofisa
Habari wa TFF, Boniface Wambura, akizuiliwa kuingia uwanjani hapo huku
walinzi waliokuwapo eneo hilo wakimueleza kuwa utaratibu umebadilika
hivyo hastahili kuingia kwa kutumia geti hilo. Baadaye aliweza kupita na
kuingia baada ya mabishano marefu.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia
Mmoja wa Wanakamati wa Yanga akizuiliwa kuingia uwanjani, askari wakimtaka kutoka nje
Benchi la Al-Ahly....
Benchi la akiba la Yanga....
Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza....
Kikosi cha kwanza cha Al-Ahly kilichoanza.....
Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, akimgalagaza beki wa Al-Ahly....
Hamis Kiiza akijaribu kumtoka beki wa Al- Ahly...
Kutokana
na mabeki wa Al-Ahly kumhofia zaidi Okwi, mara kadhaa walikuwa
wakimkaba wawili wawili na kumchezea rafu kama hivi......
Haruna Niyonzima, akiangushwa....baada ya kumramba chenga beki wa Al-Ahly
Kipa wa Al-Ahly akiruka kuokoa mchomo wa Simon Msuva.....
Mrisho Ngassa, akimramba kanzu beki wa Al-Ahly.....
Simon Msuva, akitengeneza bao la wazi kwa Hamis Kiiza ambaye alikosa.....kutokana na kuchelewa.
Shabiki wa Yanga......
Mashabiki wa Al-AHly....
Emmanuel Okwi, akiwachachafya mabeki wa Al-Ahly..
Mrisho Ngassa akijaribu kuwatoka mabeki.....
Didier Kavumbagu, akiruka na kuukosa mpira wa kichwa.....
Mrisho Ngassa, akimtoka beki wa Al-Ahly....Timu
ya Yanga leo imewashangaza waarabu wa Misri timu ya Al Ahly kwa
kuwabanjua bao 1-0, lililofungwa Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub
'Canavaro' kwa kichwa katika kipindi cha pili, mpira uliopigwa na Simon
Msuva kwa kona.
credit: mafoto blog
Post a Comment