Siku
kadhaa baada ya kutoka taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa
Uganda anayekipiga klabu bingwa ya Tanzania bara Yanga, Emmanuel Okwi
amegoma kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kuidai timu hiyo,
hatimaye leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Okwi
amevunja ukimya na kuzungumzia suala hilo.
Hiki ndicho alichoandika leo
Kwa mujibu wa Okwi sio kweli kwamba ameondoka Yanga, bali amepata
majeraha ya goti yanayomfanya asiwepo kwenye kikosi cha Yanga.
Amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa imani waliyonayo juu yake na
kuahidi kurudi dimbani kuitumikia klabu hiyo atakapopona.
Post a Comment