TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika
siku za hivi karibuni, huko mkoani Mara wilaya ya Butiama kumejitokeza
matukio ya mauaji yanayowalenga hasa akina mama wawapo katika shughuli
zao mbalimbali.
Kufuatia
matukio hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma
timu maalum ya wataamu itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa
makosa ya jinai nchini, DCI Issaya Mngulu kwenda mkoani humo kuongeza
nguvu kwa kushirikiana na wataalam wa mkoa huo, ili kuhakikisha kwamba
wote wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria haraka.
Jeshi
la Polisi linawashukuru wananchi wanaoendelea kutoa ushirikiano
utakaosaidia watuhumiwa hao kuendelea kukamatwa na linatoa wito kwa
wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo ya jirani kuwa watulivu wakati
upelelezi ukiendelea.
Aidha,
Jeshi la Polisi nchini linawaomba wananchi wenye taarifa za wahalifu
hao kutoa taarifa hizo kupitia namba za simu zifuatayo; 0715 009930,
0754 785557 au katika kituo chochote cha Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso -SSP
Msemaji wa jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso -SSP
Msemaji wa jeshi la Polisi.
Post a Comment