Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI KUHUSU MATUMIZI YA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI( EFD’S)


Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha Hassan Silayo)
 
Na Frank Mvungi
Serikali imekanusha taarifa za upotoshaji kuwa imesititisha matumizi  ya mashine za Kielektroniki ( EFD’s) hapa nchini.
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Mjanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam.
 
Akieleza Bw. Julius amesema taarifa kuwa matumizi ya mashine za kielektroniki yamesitishwa ni upotoshaji na hayana ukweli wowote.
 
Akifafanua zaidi Bw. Julius amesema kwa kuthibitisha kuwa taarifa hizo si za kweli kwani mnamo tarehe 26Februari 2014,Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda aliitisha kikao kati ya TRA,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda na biashara pamoja na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) .
 
Bw. Julius alibainisha kuwa katika kikao hicho Mh. Waziri Mkuu alielekeza kuwa orodha ya wafanyabiashara walioainishwa na kupewa barua iwekwe wazi kwa kubandikwa katika ofisi zote za TRA za Mikoa na Wilaya.
 
Pia Bw. Julius alisema kufuatia maelekezo hayo Mamlaka yaMapato Tanzania imeendelea kusimamia utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya EFds unaoendelea na orodha ya wafanyabiashara husika ipo katika mbao za matangazo ya ofisi za TRA za Mikoa na Wilaya zote pamoja na kwenye tovuti. 
Aliongeza kuwa TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini wenye sifa za kutumia mashine za kielektroniki ambao ni wa lengwa katika awamu ya pili kuzitumia kama sheria inavyotaka.
 
Bw. Julius aliwataka wananchi kutoa taarifa katika mamlka hiyo pale ambapo watatakiwa kutoa rushwa au kubugudhiwa wanapohitaji huduma katika ofisi za mamlaka hiyo kutoa taarifa katika vyombo vya dola au katika ofisi za TRA kupitia simu namba 0689122515 au ujumbe mfupi kwenye namba 0689122516. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top