|
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama
barabarani Wilaya za Rungwe na Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi
na kupokea rushwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa ni
pamoja na waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya barabara ya
Mbeya/Tunduma eneo la Songwe ni Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon.
Msangi
amewataja wengine kuwa ni pamoja Sajini Hezron,PC Shaban na PC Kajolo
ambao walikuwa wanafanya kazi barabara ya Mbeya/Rungwe wilaya ya Rungwe.
Askari
hao walikuwa wanakabiliwa na makosa hayo na walifikishwa katika
Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na kupewa
adhabu ya kufukuzwa kazi.
Aidha
Kamanda Msangi amesema Jeshi lake halitasita kuwafukuza kazi Askari
watakaokwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi na Askari yeyote
atakayekwenda kinyume atakumbwa na adhabu kali ikiwa ni pamoja na
kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani.
Askari
wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba
ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na
hatia ya wizi wa kutumia silaha,WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi
ya wizi wa mtoto.
Wengine
wliohukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuua
bila kukusudia ni DC Marcelino Venance mwenye namba 8084,PC Juma Idd
mwenye namba 3117 na Askari wa Mgambo MG Jackson Mwakalobo ambao
walidaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi Dentho Kajigili aliyekuwa
mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ivumwe ya Jijini Mbeya.
Na Mbeya yetu
|
on Monday, April 28, 2014
Post a Comment