Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA MARA MOJA MPANDA

 

???????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,  Sasi Salula akikagua moja ya miradi katika wilaya mpanda inayotekelezwa na program ya uhifadhi wa ziwa Tanganyika., hapo ni mradi wa maji ulioko kijiji cha Isengule kata ya IKola.
…………………………………………….
Na Kibada Kibada -katavi
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais,   Sasi Salula amefanya ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na ofisi yake katika ukanda wa Ziwa Tanganyika  Wilayani Mpanda Mkoani Katavi na kujionea hali halisi ya miradi  inavyoendelea kutekelezwa na kagiza kukamilika mapema iwezekanavyo.

 Agizo hilo amelitoa baada ya kukuta baadhi ya miradi ikiwa katika hali isiyoridhisha na kupata hofu kama inaweza kukamilika kwa wakati ili kwenda sawasawa na mkataba na wafadhili,  hivyo akaagiza zichukuliwe hatua za haraka kukamilisha miradi hiyo kabla ya muda kuisha.
Miradi hiyo inasimamiwa na program ya uendelezaji  na  Uhifadhi mazingira wa Bonde la ziwa Tanganyika  katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi , na makao makuu ya miradi hiyo iko mkoani kigoma na ofisi ya makamu wa Rais ndiyo inayosimamia .
Amesema watu wanaoishi Nchi zinazozungukwa na  ziwa Tanganyika wanakaribia karibu milioni kumi, na wanakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira,  hivyo hatua za makusudi zisipochukuliwa kuhakikisha mazingira ya ziwa hilo yanahifadhiwa huenda uchumi wa wananchi hao hasa wale wanaotegemea ziwa Tanganyika ukawa mashakani.
Aliitaja miradi ya inayotekelezwa kwa upande wa mkoa wa Katavi  Katika wilaya ya Mpanda ,  ukanda wa Ziwa Tanganyika kuwa ni  miradi ya Elimu , Afya, Maji na Ujenzi wa Mwalo unaojengwa kwenye kijiji cha Ikola Kata ya Ikola kwa thamani ya shilingi milioni 800,  fedha zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi wanaozunguka ukanda huo.
Akiwa katika Kijiji cha Ikola kukagua ujenzi wa Mwalo ameitaka Halmashauri kusisimamia ujenzi wa mwalo huo na kukamilika mara moja kabla ya muda uliopangwa na wafadhili  kumalizika.
Mkandarasi anayejenga mwalo ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kazi iliyofanyika hadi hapo ilipofikia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko la kuuuzia samaki, na maeneo mengine muhim
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top