Mkazi
mmoja wa kijiji cha Malili kata ya Malili Wilayani Busenda mkoani
Simiyu Japhet Nhandi(18) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya na
mnyama aina ya kiboko.
Tukio
hilo limetokea jana wilayani humo baada ya wananchi kupampana na mnyama
huyo,kitu kilichopelekea kumuua kijana huyo. Kaka wa marehemu
aliyekuwepo katika tukio hilo John Nhandi, ameiambia Blog hii kuwa tukio
hili limetokea saa 10 jioni kijijini humo wakati wa mapambano na mnyama
huyo.
Amesema
baada ya kujeruhiwa vibaya walifanya utaratibu wa kumpeleka mdogo wake
katika hospital ya rufaa ya bugando iliyopo jijini Mwanza,lakini wakati
wakiwa njiani alifariki dunia kutokana na kujeruhiwa sana na mnyama
huyo. Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Busenda Kitusi Kamani
(CCM),ambaye amehudhuria mazishi hayo kama sehemu ya mshikamano na
kuwapa pole wafiwa, amesema wanachi wilayani humo wanatakiwa kuwa makini
na wanyama pori wanaoingia kijijini humo.
Mbunge
Kamani yupo wilayani Busenda kwa mapumziko na kuendelea kuhamasisha
shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika jimbo lake. -
Post a Comment