Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata maelezo
kutoka kwa Daktari wa Kituo cha Afya Inyonga Dk. Koni,Katibu Mkuu
alitembelea kituo hicho ambacho kimeombewa kibali cha kuwa hospitali ya
wilaya tangia mwaka jana mwezi februari lakini mpaka sasa maombi
hayajajibiwa wala mkaguzi kutoka wizara ya afya hajafika kituoni
hapo,kituo hicho ni kikubwa chenye vitanda 90 na uwezo wa kulaza
wagonjwa 60 kwa mara moja,kina majengo ya kutosha na vifaa vya kutosha
kuwa hospitali ya wilaya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya vifaa vipya
kabisa vya kituo hicho cha afya cha Inyonga wilayani Mlele ambacho
kinaomba kupatiwa hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu kuendesha Pikipiki ya
kubebea wagonjwa iliyopo kwenye kituo cha afya cha Inyonga, kupewa hadhi
kuwa hospitali ya wilaya hospitali hiyo itasaidia wananchi wengi wa
wilaya ya Mlele kupata huduma karibu badala ya kusafiri umbali mrefu
mpaka wilaya ya Mpanda,hasa kupunguza sana vifo vya Mama na Mtoto.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya
Inyonga wilaya ya Mlele mkoani Katavi na kuwapongeza kwa umahiri wao wa
kuchapa kazi na kuchangia maendeleo yao na alisisitiza kuwa kero
zinazowakabili za kupata hospitali ya wilaya, maji na umeme zitatuliwa
mapema.
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi wa kata ya Inyimbo katika viwanja vya shule ya msingi Inyimbo
Vijana
wakiwa juu ya boda boda kuona mkutano vizuri mkutano wa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipohutubia kata ya Inyimbo wilaya ya
Mlele.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofali baada ya kulifyatua
kwa kutumia mashine maalum ya kufyatulia matofali wakati wa kushiriki
ujenzi wa ofisi ya CCM ,Inyimbo wilaya ya Mlele.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Katavi Dk. Pudensiana Kikwembe akibeba tofali
kusaidia ujenzi wa ofisi za CCM Inyimbo wilaya ya Mlele.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa maabara wa
shule ya Sekondari ya Kata ya Mtapenda iliyopo kata ya Nsimbo wilaya ya
Mlele.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibeba tofali wakati wa kushiriki
zoezi la kufyatua matofali ya kujenga tanki la maji katika mradi wa maji
wa kijiji cha Mwenge wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi utakaogharimu kiasi
cha shilingi milioni 400.
Post a Comment