Badhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba walio katika Umoja wa UKAWA jana jioni wameamua kutoka nje wakati wajumbe wakiendelea na majadiliano ya taarifa za kamati ya bunge hilo kuhusu sura ya kwanza na ya sita.
Hatua hiyo imefikiwa na wajumbe hao baada ya kuunga mkono mchango wa
Profesa Lipumba ambaye amesikitishwa na jinsi mjadala wa bunge hilo
unavyogubikwa na ubaguzi.
Profesa Lipumba amesema wanahitaji katiba itakayo hakikisha kila
mwananchi anapata haki yake bila kujali rangi jinsia na makabila msingi
alioucha baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Aidha Profesa Lipumba alieza kuwa amesikitishwa na Kauli iliyotolewa
na Waziri William Lukuvi wakati wa sherehe ya kumsimika mchungaji
Joseph Bundala kuwa Askofu akimwakilisha Waziri Mkuu.
Msikilize hapa:
Credit: Ibrahim Issa (Times Fm)
Post a Comment