Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao
***********
Wajumbe karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza.
Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka
kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya
wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri
Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa
serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni
uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko.
Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu kubwa.
Post a Comment