Gari alilokuwemo Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana likisindikizwa na vijana alipokuwa akiingia
Kata ya Mwandiga, Wilaya ya Kigoma, leo Katibu Mkuu huyo akiwa katikaa
ziara ya siku tano mkoani Kigoma kukagua na kuimarisha uhai wa chama na
kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM
Kinana akilakiwa baada ya
kuwasili kwenye Ofisi ya CCM, Kata ya Mwandiga, Kigoma Vijijini ambapo
alifamya mkutano wa ndani na Kamati ya Siasa ya Kata hiyo.
Kiongozi wa Madereva wa Daladala
Stendi ya Mwandiga, Kigoma, Bagaya Mustafa ambaye ni mwanachama wa
Chadema, akiwashawishi wakazi wa eneo hilo kujiunga na CCM, baada ya
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno, kusitisha operesheni ya
Sumatra kuwakamata madereva wasio na sare na kuwatoza faini kubwa,
kitendo ambacho kilisababisha kuitisha mgomo wa daladala kati ya Kigoma
Mjini na Mwandiga leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye aliyemwelekeza Maneno kutoa sitisho hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma,
Ramadhan Maneno akitangaza kusitisha operesheni operesheni hiyo
iliyokuwa inafanywa na maofisa wa Sumatra kwa ushirikiano na polisi.
Kinana akiongozana na viongozi wengine wa CCM na Serikali alipokagua mradi wa wajasiliamali wa kilimo Kigoma Vijijini.
|
Ayub Kabwe ambaye ni Katibu wa
Uenezi wa Wilaya ya Kigoma Vijijini, ambaye pia ni babake mdogo wa
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Jimbo la Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe, akihamasisha wananchi wakati wa ziara ya Kinana
katika mji wa Mwandiga ambao ni nyumbani kwaa Zito.
Watoto wakigombea kuteka maji ya kisima cha mradi huo wa maji
Vijana wakitumbuiza kwa ngoma
wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
katika Kijiji cha Mahembe, Kata ya Mahembe leo.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara
katika Kata ya Mahembe, Jimbo la Kigoma Kaskazini.
|
Nape akisisitiza jambo katika
mkutano huo, ambapo alimchanachana Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe (Chadema), kwa kutowajali wapigakura wake bali kuyapigania
masuala ya kimastaifa, kama vile masuala ya Buzwagi, viongozi wanaoficha
fedha njie ya nchi, badala ya kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi kama vile maji, sekta ya afya, barabara na
elimu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaburu akihutubia kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Kinana.
Kinana akisoma orodha ya vijiji
vitakavyopatiwa umeme na maji katika wilaya ya Kigoma Vijijini.
Kikiwemo Kijiji cha Mahembe ambacho tayari kimepata umeme.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo
Wanachama wapya wa CCM wakila
kiapo cha utii wakati wa mkutano huo wa hadhara katika Kata ya
Mahembe.Zaidi ya watu 160 walijiunga na chama hicho.
Wananchi wakinyoosha juu mikono kula kiapo cha utii cha CCM
Kinana akiongea na mtu mwenye ulemavu aliyehudhuria mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe
Post a Comment