Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25
vimethibitishwa na ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu
wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala, vilitokea vifo 11 ingawa
inahisiwa watu wengine wawili hawaonekani. Kinondoni vifo ni saba huku
wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke vifo
saba.
Sadiki alitaka uchunguzi wa
polisi ufanyike kila familia
zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo
14 vilitokana na mafuriko.
Kuhusu kurudi katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.
Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani inasubiri uamuzi
wa mahakama kutokana na kuwepo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake
Post a Comment