Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mambo matatu kuhusu Mtoto aliebaki na risasi kichwani baada ya shambulio Mombasa

Screen Shot 2014-04-02 at 4.02.02 AM
Ni mtoto Satrin Osinya ambae mama yake mzazi aliuwawa kwenye shambulio lililofanywa kanisani huko Mombasa Kenya ambapo watu waliokua na silaha walishambulia kwenye ibada ikabidi mama amkinge mtoto, ikisemekana risasi iliyofyetuliwa ikamuua mama na kupenyeza mpaka ikagota kichwani kwa mtoto aliebaki hai.
Satrin mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita alibaki na hiyo risasi kichwani toka shambulio hilo lilipotokea zaidi ya wiki moja iliyopita.
Screen Shot 2014-04-02 at 3.55.13 AM
1. Madaktari katika hospitali ya Kenyatta Nairobi Kenya wamefanikiwa kuitoa risasi hiyo April 1 2014 baada ya kazi ya dakika 180 ambapo sasa mtoto huyu hayupo tena kwenye hatari ya kupoteza maisha.

2. Kikundi cha Madaktari 12 bingwa wa kichwa ndio kimeifanya hii kazi.
3. Madaktari wanasema mtoto huyu ameanza kuongea, kucheza na hata kusogea tofauti na mwanzo.
Hapa Satrin akiwa amebebwa na kaka yake
Hapa Satrin akiwa amebebwa na kaka yake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top