Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAN UNITED SARE 1-1 NA BAYERN PUNGUFU OLD TRAFFORD, BARCELONA NAYO YASHIKWA NYUMBANI NA ATLETICO

 

Lingekuwa la ushindi; Nemanja Vidic akiifungia Man United bao la kuongoza usiku huu Uwanja wa Old Trafford

*******


MANCHESTER United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Bayern Munich katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford mjini Manchster, England.
United walikuwa wa kwanza kupata bao lao dakika ya 58 lilifungwa na Nahodha Nemanja Vidic kwa kichwa cha nyuma akimalizia kona ya Wayne Rooney.

Iliwachukua dakika nane tu mabingwa wa Ulaya kuchomoa bao hilo, mfungaji Bastian Schweinsteiger aliyemalizia kazi nzuri ya Mario. Mandzukic dakika ya 66.
Mapema kipindi cha kwanza, Danny Welbeck alikosa bao la wazi akiwa yeye na kipa Manuel Neuer akaokoa, wakati kabla ya hapo alimnawisha mpira Javi Martiezn na kufunga bao ambalo lilikataliwa na refa.
Mshambuliaji wa Bayern Bastian Schweinsteiger alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei kwa kumchezea rafu Rooney.
Kwa matokeo hayo, United sasa inahitaji ushindi katika mchezo wa ugenini Aprili 9, mwaka huu.
Katika mchezo mwingine wa Robo ya michuano hiyo usiku huu, Barcelona ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid Uwanja wa Camp Nou.
Diego Coasta alitangulia kuifungia Madrid dakika ya 56 Gabriel ‘Gabi’ Fernandez Arenas, kabla ya Neymar da Silva Santos Junior kuisawazishia Barca dakika ya 71 pasi ya Andres Iniesta.
Barca sasa inahitaji ushindi katika mchezo wa marudiano ugenini Aprili 9, mwaka huu.
Imecotwa: Bin zubery web
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top