JKT Oljoro iliyoifumua Prisons Mbeya mjini Arusha |
Mgambo inayoendelea kutesa timu kongwe kwa kuifunga Coastal 2-0 mjini Tanga |
Rhino Rangers wameifanyia maajabu Mtibwa kwa kuilaza bao 1-0 |
TIMU zilizopo katika hatari ya kushuka
daraja, Oljoro JKT, Mgambo JKT na Rhino Rangers zimeibuka na ushindi
katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ushindi wa timu hizo umezidi kufanya
kinyang'anyiro cha timu za kutaka kushuka daraja kuzidi kunoga kwani
hakuna aliyena uhakika mpaka sasa wa kushuka au kubakia katika ligi hiyo
mpaka sasa ligi ikiwa kwenye raundi ya 24.
Mgambo ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani ilipepetana na Coastal Union na kupata ushindi wa mabao 2-0.
Mabao ya washindi walitoka kuifumua Yanga wiki iliyopita yaliwekwa kimiani na Peter Malianzi, Boli Ajali
na
'Wazee wa Oman' wakishindwa kufurukuta kwa maafande hao ambao
wamejiweka katika nafasi nzuri ya kupona kuteremka Ligi Daraja la
Kwanza.
Katika
mechi nyingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
wenyeji waliopo nafasi ya pili toka mkiani wakipata ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya maafande wa Prisons-Mbeya, huku Rhino inayoburuza mkia
ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ligi
hiyo itaendelea tena siku ya Jumatano kwa mechi ambazo zinaweza kuamua
hatma ya ubingwa baona ya Yanga na Azam, wakati timu hizo zitakapokuwa
viwanja viwili tofauti.
Yanga
itakuwa uwanja wa Taifa kupepetana na Kagera Sugar wakati Azam
itawafuata Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi.
Azam
inaoongoza msimamo kwa pointi 53 na Yanga iliyoifumua JKT Ruvu jioni
hii mabao 5-1 inafuatia ikiwa na pointi 49 na Mbeya inafuata na pointi
36 katika nafasi ya tatu, kisha Simba yenye pointi 37.
Post a Comment