Shughuli
za uchukuzi wa mizigo toka bandarini kwenda mikoani na nchi za jirani
kwa njia ya reli ya Tazara zitasimama kwa siku saba,kufuatia maji ya
mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar-es-Salaam,kusomba tuta la reli ya
tazara umbali wa mita arobaini na kuacha mataruma ya reli hiyo
yakining'inia.
Meneja
mkuu wa mkoa wa mamalaka ya reli ya Tanzania na Zambia Tazara, mhandisi
Abdalah Kimweri amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha jijini
Dar-es-Salaam,zimeathiri miundombinu ya mamlaka hiyo umbali wa kilometa
nane kati ya maeneo ya kurasini na yombo jijini Dar-es-Salaam.
Mhandisi
huyo medai kuwa,katika maeneo mengi inapopita reli hiyo hasa jijini
Dar-es-Salaam,makambako mkoani njome na tunduma jijini mbeya baadhi ya
wananchi wamejenga karibu kabisa na reli hiyo jambo ambalo ni hatari
kwao na kwa reli ya Tazara na kudai kuwa tayari wameisha wajulisha
wananchi kuondoa maendeleo yao kabla ya hatua kali za kisheria
hazijachukuliwa dhidi yao.
Mhandisi
ujenzi wa mamlaka hiyo ya Tazara kwa upande wa Tanzania mhandisi
Richard Festo,amesema kuwa katika maeneo ya temeke jijini
Dar-es-salaam,ujenzi holela wa mfumo wa mitaro kuelekezewa kupita kwenye
njia ya reli kumechangi kwa kiasi kikubwa kuchangia kuharibu
miundombinu ya mamlaka hiyo,huku baadhi ya wananchi wakitaka kulipwa
fidia kwa makaburi yao yaliyosombwa na maji.
Reli
ya tazara yenye historia ya urafiki baina ya nchi tatu za Tanzania
,Zambia na uchina ikiwa na urefu wa kilometa 1860 kutoka jijini
Dar-es-salaam nchini Tanzania hadi new kaplimposhi nchini Zambia
,iliyoanza kutumika kusafirisha abiria na mizigo kwenye mikoa ya
Pwani,Morogoro,Iringa na Mbeya iliyo anza kutoa huduma hiyo mwanzaoni
mwa miaka ya 1976 ikiwa imejengwa na kampuni kutoka China.
Chanzo ITV Online
Post a Comment