Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWALIMU SHULE YA MSINGI LOLE KATA YA IKUNA NJOMBE AUAWA KIKATILI

RPC
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Akizungumza na Mtandao huu.
Na Gabriel Kilamlya Njombe

Licha Ya Jeshi la Polisi Kuendelea Kukabiliana na Matukio Ya Mauji Ya Kulipizana  Visasi na Imani za Kishirikina Lakini Matukio Ya Mauaji Ya  Kutisha Yanaendelea Kushamili Mkoani Njombe Siku Hadi Siku Hali Inayohatarisha Ustawi wa Maisha Ya Wakazi wa Mkoa wa Njombe

Machi 30 Mwaka Huu Huko Katika Kijiji cha Lole Kata ya Ikuna Wilayani Njombe Yametokea Mauaji Ya Kutisha Baada Ya Mwalimu wa Shule Ya Msingi Lole Kuuawa Kikatili.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kwamba Majira Ya Saa 4:30 Usiku Katika Kijiji Hicho Cha Lole  Mwalimu wa Shule Ya Msingi Lole Luchabiko Ngimbudze Mwenye Umri wa Miaka 55 Aliuawa na Mtu/Watu Wasiofahamika Kwa Kupigwa na Kitu Kizito Usoni.

Taarifa Ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Imeeleza Kuwa Baada ya Mwalimu Huyo Kupigwa na Kitu Kizito Usoni Pia  Alifungwa  na Shati Shingoni.
 
Taarifa Hiyo Imefafanua Kuwa Marehemu Aliuawa Baada ya Wauaji Hao Kuvunja Mlango wa Nyumba Yake na Kuingia Ndani Hadi Chumbani Kwake.

Katika Hatua Nyingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Amesema Kitendo cha Wananchi Kuendelea Kujichukulia Sheria Mkononi Hakifai Katika Jamii na Hivyo Kinapaswa Kupigwa Vita Kwa Kila Mmoja Wetu.

Hata Hivyo Jeshi Hilo Limetoa Wito Kwa Mtu Au Watu Wenye Taarifa Ya Watu Waliohusika na Tukio Hilo Ili Hatua Za Kisheria Ziweze Kuchukuliwa Dhidi Yao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top