Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RONALDO AIKAMATA REKODI YA MESSI BARCA IKIICHAPA 3-0 DORTMUND, CHELSEA YAKALISHWA

REAL Madrid imebisha hodi Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borrusia Dortmund usiku huu kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu katika Robo Fainali ya kwanza ya michuano hiyo.
Gareth Bale alifunga bao la kwanza dakika ya nne akimchambua vizuri Weidenfeller baada ya kazi nzuri ya Karim Benzema.
Asante Mungu; Ronaldo akishangilia bao la tatu aliloifungia Real Madrid ikiua 3-0 Borrusia Dortmund na kufikia rekodi ya mabao ya Messi Ligi ya Mabingwa Ulaya na chini ni Gareth Bale akishangilia bao la kwanza

Isco akafunga la pili dakika ya 27 baada ya kazi nzuri ya Benzema tena na Mreno Cristiano Ronaldo akafunga la tatu dakika ya 57 kwa pasi ya Luka Modric. 
Bao hilo linamfanya Ronaldo aifikie rekodi ya hasimu wake, Muargentina wa Barcelona, Lionel Messi kufunga mabao 14 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
Borrussia sasa watahitaji ushindi wa mabao 4-0 ili kufufua matumaini ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo- au washinde 3-0 ili mshindi aamuliwe kwa mikwaju ya penalti.
La ushindi; Beki David Luiz akimtungua kipa wake mwenyewe Petr Cech kuipatia PSG bao la ushindi

Katika mchezo mwingine, Chelsea imefungwa mabao 3-1 na wenyeji PSG Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.
Bao lililoizamisha timu ya Mreno Jose Mourinho usiku huu alijifunga beki wake, David Luiza dakika ya 62 katika harakati za kuokoa krosi ya Ezequiel Lavezzi.
PSG walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne baada ya Lavezzi kutumia vizuri makosa ya beki John Terry na kumtungua kipa Petr Cech kabla ya Javier Pastore kufunga la tatu dakika ya 90 na ushei.
The Blues walisawazisha kwa penalti dakika ya 27, mfungaji Eden Hazard akimchambua vizuri Salvatore Sirigu baada ya Thiago Silva kumchezea faulo Oscar kwenye eneo la hatari.
Chelsea itarejea Stamford Bridge wiki ijayo ikihitaji ushindi wa 2-0 tu ili kwenda Nusu Fainali baada ya matokeo ya leo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top