NYUMBA
ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Bavicha), John Heche, iliyopo Mabibo Loyola, jijini Dar es
Salaam, imevamiwa na watu wasiojulikana, ambapo vitu vyenye thamani ya
zaidi ya sh milioni 10 vimeibwa.
Tukio
hilo limetokea wiki iliyopita muda mfupi baada ya Heche kutoka
nyumbani kwake alfajiri kwenda katika kituo cha mabasi ya mikoani cha
Ubungo, kuwahi usafiri wa kwenda jijini Mwanza.
Tayari
tukio hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi Mabibo Mwisho na
kupewa kumbukumbu namba MAB/RB/225/2014, kabla ya kuhamishiwa katika
Kituo cha Polisi Urafiki na kupewa namba URP/RB/2785/2014.
Hata
hivyo tukio hilo limeanza kuhusishwa na masuala ya kisiasa hususan
katika vitu vinavyodaiwa kuibwa na namna Jeshi la Polisi Kituo cha
Urafiki wanavyolishughulikia.
Vitu
vilivyoibwa ni pamoja na Friji, radio, TV, Decoder ya Dstv, jezi za
mpira jozi 32, mipira 56, magodoro, meza ya TV na music system
inayotumika kwenye mikutano ya hadhara.
Hadi
sasa tayari mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kuhusika na tukio hilo
amekamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo pamoja na wenzake ambao bado
wanaendelea kusakwa.
“Yule
aliyekamatwa amekiri mbele ya Polisi kuhusika na tukio na akawataja
wengine sasa tunashangaa kigugumizi cha Polisi katika hili ni nini mpaka
wanashindwa kuwafuatilia na kubaini sababu zilizowafanya waibe hapa,”
alisema mmoja wa majirani wa Heche.
Kauli ya Heche
Heche
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipoulizwa iwapo anaweza
kulihusisha tukio hilo na shughuli zake za kisiasa, alisema ni mapema
kuhusisha tukio hilo na siasa moja kwa moja.
“Silihusishi
moja kwa moja na siasa lakini namna askari wa Kituo cha Polisi Urafiki
wanavyolichukulia kiwepesi ndiyo inanipa shaka,” alisema Heche
Kauli ya RPC Wambura
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura, alipoulizwa kama
analijua tukio hilo alisema hana taarifa nalo na kwamba atafuatilia
kujua kama lipo.
>>>>>Tanzania daima
>>>>>Tanzania daima
Post a Comment