Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shambulizi la kigaidi lawaua 6 Kenya

 



Watu sita wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi.
Polisi wamesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha mabomu katika mkahawa mdogo ulio karibu na kituo cha mabasi mtaani humo.
Walioshuhudia shambulizi walisema kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha hilo.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa na washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.
Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.
Inaarifiwa washambuliaji walitumia maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo.Chanzo BBC Swahili
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top