Baadhi ya wagonjwa wakiwa wametolewa hospitali ya TMJ baada ya nyumba ya jirani kuwaka moto. Walitolewa wodini kwa tahadhari.
Kikosi
cha Kuzima Moto kikizima moto nyumba jirani na Hospital ya TMJ iliyopo
Mikocheni Dar es Salaam muda huu na watu kudhani kuwa iliyokuwa ikiungua
ni hospitali.
Wagonjwa wakitolewa nje na manesi wa Hospital ya TMJ baada ya nyumba jirani kuwaka moto.
Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar
es Salaam ilizushiwa kuwaka moto baada ya nyumba jirani kulipuka moto,
hali iliyosababisha hekaheka kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo ya
kuwatoa nje wagonjwa kwa tahadhari.
Tahadhari hiyo ilichukuliwa kutokana
na wasiwasi kuwa moto huo ungeweza kuvuka na kuingia hospitali lakini
ulidhibitiwa na kikosi cha zima moto na kuishia katika nyumba hiyo ya
jirani.
Post a Comment