Salumu
Abel Muhunda mkazi wa Kata ya Cheyo manispaa ya Tabora amejeruhiwa
vibaya na kundi la Majambazi ambayo yalimvamia wakati akiuza dukani huko
eneo la Mwanga Shop ambapo majambazi hayo yalivamia yakiwa na bunduki
na kufyatua risasi hewani huku yakimjeruhi kwa kumpiga mapanga na nyundo
kichwani na baadae kumpora kiasi kikubwa cha fedha.
Muhunda
ambaye kwasasa amelazwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ni
mmoja kati ya watu walioathirika na matukio ya unyang'anyi wa kutumia
silaha unaofanywa na majambazi hayo ambayo hufanya unyama huo kila siku
na kwasasa takribani miezi mitatu mfululizo eneo la manispaa ya Tabora
waathirika wakubwa ni wafanyabishara ya maduka madogo ya mitaani pamoja
na M-pesa.
Credit: Kapipi
Post a Comment