Watoto wawili wa kiume wa familia
moja, Daniel Paul (8) na mdogo wake, Emmanuel Paul (3), wamepoteza
maisha wakiwa pamoja baada ya kuteketea kwa moto ndani ya nyumba.
Tukio hilo lilijiri majira ya saa 1:00 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa
Rufita, Mwanza-Road mjini Tabora baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi
kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani.
Habari za awali zilieleza kuwa chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni
hitilafu ya umeme na kuisababishia familia hiyo majonzi makubwa ya
misiba miwili kwa mpigo.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora, OCD, Samwel Mwampashe alithitisha
kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa polisi watafanya uchunguzi ili
kubaini chanzo kamili cha moto huo
Post a Comment