Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akiwasili Ukumbini hapa Maryland kufungua Shina la Chama cha Mapinduzi hii leo.
Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia Jambo na
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-DMV wakati akiwasili kwenye Uzinduzi wa
Shina la CCM-Maryland.
Naibu
katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiwapungia Mkono Wana-CCM
waliofika kwenye Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland hapa Marekani.
Comrade
Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
waliofika kwenye tukio la Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na
MC wa Shughuli ya Ufunguzi wa Shina la CCM akiwajibika kuweka ratiba sawa Ukumbini,Makada watiifu wa Chama cha Mapinduzi hapa Maryland.
Watanzania na Wana-CCM wakiwa tayari Kuitumikia Nchi yao na Chama chao.
Wadau wakipata Ukodak.
Mh:Mwigulu
Nchemba akipokea kadi ya aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA ambaye ameamua
Kuachana na Chama hicho na Kujiunga na Chama cha Mapinduzi,
Loveness
Mamuya kada Mtiifu wa CCM na Muasisi wa harakati za CCM hapa Marekani
akiwasalimia wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliofika kwenye Uzinduzi
wa Shina la CCM Maryland.
Mwenyekiti
wa CCM Kwa Watanzania waliopo DMV akizungumza na Wana-CCM Umuhimu wa
Kujiunga na Chama cha Mapinduzi,Pia amezungumzia Maadili ya Watanzania
wanaoishi nje ya Nchi hususani Marekani Kutukana Viongozi Mitandaoni"Huo
sio Utamaduni Wetu Watanzania" alisema.
Wana-CCM Wakipata Ukodak.
Hapa ni Mwendo wa CCM nambari One.
Makada Watiifu wa Chama cha Maopinduzi hapa Maryland.
Sehemu
ya Wana-CCM waliofika kwenye Uzinduzi wa Shina la CCM Maryland
wakisikiliza kwa makini Ujumbe kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Mh:Mwigulu
NChemba.
Makada wa Chama cha Mapinduzi wakipata Ukodak.Mama Nchemba (Mke wa Mh:Mwigulu) akisalimia Wana-CCM waliofika Kwenye hafla ya Uzinguzi wa Shina la CCM Marly Land
Miss Temeke akiwa na Mmewake kwenye uzindui wa Tawi la CCM-Maryland.Mwanachama
wa CCM akiuliza Swali kwa Mh:Kuhusu Urai Pacha na namna Chama cha
mapinduzi kilivyolichukulia Swala hilo.Mh:Mwigulu Nchemba amesema Chama
cha Mapinduzi kwenye rasimu mpya Kimependekeza Urai pacha na Kimejipanga
Kuhakikisha jambo hilo linachukuliwa kwa Uzito wake na hatimaye Uraia
pacha Upatikane.
Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia jambo
mara baada ya Mwanachama wa CCM kusema kutokana na Mwenendo wa Siasa
zake atakuwa kuwa Kiongozi Mkubwa katika Nchi hii,na Wana-CCM
wataendelea Kumuunga Mkono katika kazi zake.Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-DMV -CCM akitoa Ombi rasmi kuwa Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba awe mlezi wa Jumuia ya Wanawake=DMV.
Mh:Mwigulu Nchemba akishiriki Chakula kilichoandaliwa kwenye hafla ya Ufunguzi wa Shina la CCM-Marland-Marekani.
Mwenyekiti wa Shina la CCM-Maryland Ndugu Mrisho Mzese akishiriki Chakula kilichoandaliwa kwenye Ufunguzi huo wa shina.Furaha ya Kukutana na Kiongozi wa Kitaifa ni pamoja na Kuweka Kumbukumbu ya Picha kama hivi.Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wanawake-CCM hapa Marekani(Watatu kutoka Kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wanawake walifika kwenye hafla ya
Uzinduzi wa Shina la CCM-Maryland.
Viongozi wa Chama wakiongozwa na Naibu
Katibu Mkuu-CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba kupiga picha ya pamoja na
Wanachama wapya wa Chama cha mapinduzi.Hii leo Mh:Mwigulu Nchemba
amepokea Wanachama 8 wapya waliojinga na CCM.
Kutoka Washington-DC.
Naibu katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu
Nchemba hii leo tar 27/04/2014 amezindua Shina la Chama cha Mapinduzi
hapa Maryland tayari kwa kuanza kuitumikia CCM na Wanachama
wake.Ufunguzi wa Shina hili ni mwendelezo wa kuhakikisha Wanachama wa
Chama cha Mapinduzi wanakuwa katika Mfumo mmoja wa Kichama.
Akizungumza na Watanzanai waliofika
kwenye Uzinduzi huo,Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kwa Wana-CCM
wanatakiwa kujenga mazingira ya Kuwa pamoja mara kwa Mara kwaajili ya
Kujenga Umoja na Mshikamano hasa Ukizingatia wapo Mbali na Nyumbani
Tanzania.
"Umoja wenu ndio Ngao yenu kwa hapa
Marekani,Naomba sana Mshiriki kwenye Jumuia zenu na mshiriki kwenye
Shughuli za pamoja zikiwamo hizi za Kisiasa,Haitakuwa afya Kufunga
Mashina na Matawi ya CCM Kwaajili ya Kuvunja Umoja wetu,Tutumie Mashina
haya Kutuimarisha zaidi"alisema Nchemba.
Mbali na hilo na Kudumisha
Umoja,Mh:Nchemba ameendelea kusisitiza kuwa Mchakato wa Katiba Mpya ni
jambo Zuri sana lakini Kukosekana kwa Utashi wa Kisiasa kwa Viongozi wa
Kisiasa kunapeleka katiba ama kutopatikana au Kuchelewa kupatikana.Hivyo
ameomba Watanzania waliopo Marekani na Nchi nyingine kaucha kushabikia
Mambo yasiyokuwa na tija kwa Taifa lao ambayo yatapelekea Utengano.
Zaidi ameahidi Viongozi wa CCM
Wataandaliwa Semina kwaajili kupata Mafunzo ya Kuwa Kiongozi Mwadilifu
na Mzalendo kwa Chama na Taifa letu.
Picha/Maelezo na Sanga-Festo /Washington DC
Post a Comment