Na Mwandishi Wetu
Warembo watakaoshiriki
kwenye shindano la kusaka mrembo wa Tabata 2014, watatambulishwa leo katika
ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo
Joseph Kapinga alisema jana utambulisho huo utaenda sambamba na kusherekea
sikukuu ya Pasaka.
Kapinga alisema bendi ya
African Stars “Twanga Pepeta” itasindikiza uzinduzi huo utakaojumuisha pia
washiriki wa Miss Ukonga na Miss Mzizima wa mwaka huu.
Pia Kapinga alisema kuwa
Twanga Pepeta pia itatumia utambulisho huo kutambulisha nyimbo zao mpya kama
zawadi yao ya Pasaka kwa wapenzi wao.
Alisema bendi hiyo
ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi
majogoo.
Mratibu huyo alisema wapenzi
wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao leo kabla hawajashiriki kwenye
shindano la kumsaka Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi
ujao.
Pia watakuwepo viongozi waandamizi
kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss
Tanzania Happiness Watimanywa pamoja na Miss Tabata Dorice Mollel.
Washiriki wa Miss Tabata
ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20),
Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes
Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na
Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wenine ni Annatolia
Raphael (21), Mary Henry (21), Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail
(20), Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi
(21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na
Ramta Mkadara (20)
Warembo hao
wanafundishwa na Neema Chaki na Pasilida Bandari. Warembo watano kutoka
Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka
huu.
Mrembo anayeshikilia
taji la Miss Tabata ni Dorice Mollel ambaye pia ni Redds Miss Ilala.
Utambulisho
umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa
Konyagi, Saluti5 na Father Kidevu Blog (www.mrokim.blogspot.com
CREDIT: Father Kidevu Blog
Post a Comment