Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

YULE MTOTO SATRINE AONDOLEWA RISASI KICHWANI




Kakake Satrine akimpakata Satrine hospitalini kabla ya kufanyiwa upasuaji Nairobi
Madaktari katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini Kenya,Kenyatta, wamefanikiwa kuondoa risasi iliyokuwa imekwama katika ubongo wa mtoto Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Risasi hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo iliyomuua mamake.
Mamake Satrine alikuwa amempakata mtoto wake ili kumlinda kutokana na magaidi waliovamia kanisa walimokuwa wiki moja iliyopita katika mtaa wa Likoni mjini Mombasa.
Lakini walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo huku risasi iliyomuua mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye ubongo wake.
Satrine alipelekwa Nairobi kwa matibabu maalum kutoka Mombasa kutokana na ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.
Shughuli ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na ilifanywa na madaktari watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu wa kitengo cha upasuaji wa neva katika hospitali hiyo.
Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema hawakupata matatizo walipokuwa wanafanya upasuaji huo.

SOURCE:BBC
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top