ANDRES
Iniesta anaamni Gerardo Martino ndiye kocha bora anayeifaa Barcelona
kwasasa licha ya kuwepo tetesi kuwa ataondoka majira ya kingazi mwaka
huu.
Kocha wa Celta, Luis Enrique anaripotiwa kumrithi Martino aliyerithi mikoba ya marehemu Tito Vilanova msimu uliopita.
Kutolewa
hatua ya robo fainali ya UEFA, kupigwa na Real Madrid katika fainali ya
Copa del Rey na kushindwa kuongoza La Liga kumemuweka kitimoto Martino,
lakini Iniesta amemtetea kuwa anajua kufundisha.
“Kwa
upande wangu, kocha tuliyenaye kwasasa ndiye bora,” Iniesta aliwaambia
Diario Ole. “Pia nitafurahi sana kuona anakaa kwa muda mefu zaidi na
kuonesha uwezo wake wote”.
“Msimu wa kwanza ni mgumu kwa kila mtu. Nimeona akiwa na nia na mipango mizuri. Siku zote anatuamini”.
‘Wakati
fulani mambo hayaendi kama unavyotaka, lakini unatakiwa kujaribu.
Ulimwengu wa Barcelona ni mgumu sana, sio kwake tu, hata sisi
wachezaji”.
“Tumeshindwa kufanya vizuri katika nyakati muhimu. Wakati fulani mambo yanakwend vibaya”.
“Sio
kwamba unataka hivyo, ni kwasababu wakati mwingine inatokea. Unatakiwa
kufanya mabadiliko bila kujali unashinda mataji au hushindi”.
Barca
watasafiri kesho kuwafuata Elche katika mchezo wa La Liga na kushinda
kutawapa nguvu kubwa ya kutwaa ubingwa mbele ya wapinzani wao, Atletico
Madrid.
Loading...
Post a Comment