Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KONGAMANO LA UWEZESHAJI BIASHARA KWA NCHI CHANGA ZA AFRIKA KUANZIA TAREHE 14 MPAKA 16 MEI, 2014-MWANZA.

4386846841_f341c7cdf7
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
TAARIFA KWA UMMA.

Mkutano Mkuu wa 9 Ngazi ya Mawaziri katika Shirika la Biashara la Dunia “World Trade Organization (WTO)” uliofanyika kutoka tarehe 3 hadi 6 Desemba, 2013 katika mji wa Bali, Indonesia uliazimia kuboresha taratibu za kiforodha ili zifanyike kwa haraka na ufanisi mkubwa kuliko ilivyo ilivyo sasa kupitia ushirikiano kati ya mamlaka za forodha za nchi wanachama.
Makubaliano hayo pia yamechukua mahitaji ya Nchi zinazoendelea na zile zilizo changa kama vile Tanzania kwa kubeba misimamo ya msaada wa Kiufundi na kujenga uwezo katika Uwezeshaji Biashara.

Kwa kutambua fursa zilizo ndani ya Makubaliano ya Uwezeshaji Biashara na changamoto zinazozikabili Nchi changa katika utekelezaji wa makubaliano hayo, Serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na “East African Research Capacity Development Foundation (EARCDF)”, “Nordic Africa Institute (NAI) of Sweden” na “SITRADE” imeandaa Kongamano la siku 3 ambalo linafahamika kama “kongamano la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa bali kwa nchi changa za afrika kuanzia tarehe 14 mpaka 16 Mei, 2014 katika Hoteli ya Snow Gold Crest Mwanza, Tanzania.

Kongamano hili litahudhuriwa na Vionngozi na Maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania, Mabalozi  Modest J. Mero (Ubalozi wa Kudumu Tanzania, Geneva) ambaye kwa sasa ni Msemaji (Negotiator) na Mratibu katika maswala ya Uwezeshaji Biashara katika Shirika la Biashara la Dunia (WTO) kwa niaba ya Nchi Changa; na Balozi Ali Mchumo (Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la WTO).

Pia watakuwepo Wajumbe 22 wa Nchi changa za Afrika ambazo ni mwanachama wa Shirika la WTO. Washiriki wengine watakuwa takribani 40 ambapo idadi yao inajumuisha wataalam waliobobea katika maswala mbalimbali, wakiwemo watafiti wa maswala ya Biashara na mameneja wa Sera za Biashara kutoka katika ngazi za juu.

Kongamano hili linalenga kuakisi Agenda ya Uwezeshaji Biashara baada ya Bali ambapo ndani yake kuna masuala muhimu na mpango kazi kwa Nchi Changa za Afrika. Dhima hii inalenga maeneo muhimu ambayo ni:
  1. Uelewa katika mtazamo wa kihistoria, dhana, msingi na hatua mbalimbali ambazo dhana ya Uwezeshaji Biashara imepitia
  2. Hali ya muonekano wa Uwezeshaji Biashara katika Jumuiya za Uchumi Kikanda Afrika “Trade Facilitation in African Regional Economic Communities (RECs)”;
  3. Kutumia uzoefu utakaokuwa umepatikana ili kutengeneza mapendekezo ya agenda kazi ya utekelezaji wa makubaliano ya WTO katika Uwezeshaji Biashara.
Imetolewa na,
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
DAR ES SALAAM

MEI 12, 2014.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top