Kiingilio
cha chini cha mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili (Mei 18
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Washabiki
watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya
rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio
kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Tiketi
zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi hiyo katika vituo
mbalimbali jijini Dar es Salaam, na uwanja siku ya mchezo huo utakaoanza
saa 10 kamili jioni.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
Mart Nooij inatarajia kurejea jijini Dar es Slaam kesho (Mei 14 mwaka
huu) kutoka Mbeya kuendelea na maandalizi ya kuikabili Zimbabwe.
Post a Comment