Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rsami na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Ndugu Ahmed Kipozi mara baada ya kuwasili kwenye Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Mandera iliyoko wilayani Pagamoyo tarehe 10.5.2014.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy
akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye
shule hiyo tarehe 10.5.2014.
]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]]
Mke wa
Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera
akisalimiana na baadhi ya walimu wa Shule hiyo mara alipowasili shuleni
hapo kwa ziara ya siku moja tarehe 10.5.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi (kulia) na wageni wengine wakitembelea
maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia jaribio la somo la Fizikia (Hooke’s
Law: Inayosema ‘The force needed to extend or compress a spring by some
distance is proportional to that distance’) lililokuwa likifanywa na
mwanafunzi Mwajuma Mwanankuta wa Kidato cha 4 katika Shule ya Sekondari
ya wasichana ya Mandera tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ya saluti ya Girl Guides kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Mandera .
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko
Wilayani Bagamoyo wakiimba wimbo wa shule kwa ajili ya kumkariisha Mlezi
wa shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shule hiyo tarehe
10.5.2014.
Mkuu
wa Shule ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy akimkabidhi risala
Mlezi wa Shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shuleni hapo tarehe
10.5.2014.
Mke wa
Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko
wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani Mama Salma Kikwete akizungumza na
wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
shule tarehe 10.5.2014.
Daktari
Hadija Mwamtemi aliyefuatana na Mama Salma Kikwete anaonekana
akimhudumia mwanafunzi (jina lake halikuweza kupatikana) wa Shule ya
Sekondari ya wasichana ya Mandera aliyekuwa mgonjwa wakati Mama Salma
alipotembelea shuleni hapo tarehe 10.5.2014.
Mke wa
Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Mama Salma
Kikwete akiw\ katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule
hiyo na baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya Mama Salma kuongea na
wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo tarehe 10.5.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Post a Comment