Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MIKATABA YA MAMILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA YASAINIWA MKOANI NJOMBE


Mkandarasi wa Kampuni Ya Boimanda Akisaini Mkataba wa Shilingi Milioni 68 wa Ukarabati wa Barabara Kuelekea Ludewa Tayari Kwa Uchimbaji Makaa ya Mawe na Chuma Liganga
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe Awashtua Wakandarasi Watakaoharibu Kazi Kuwa Atachongea Bungeni.
====
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe Amesema Hatosita Kupaza Sauti Yake Bungeni na Kuwatupia Lawama Wakandarasi Watakaojenga Barabara Za Ludewa Chini Ya Kiwango  Hususani Zinazoelekea Katika Migodi Ya Makaa Ya Mawe na Mchuchuma Liganga.
Kauli Hiyo Ameitoa  Wakati Serikali Mkoani Njombe Ilipokuwa Ikisaini Mikataba na Wakandarasi Wanne Watakaofanya Kazi Ya Kulima Barabara Ya Kuanzia Itoni Hadi Kwenye Makaa ya Mawe na Liganga Huko Mchuchuma Wilayani Ludewa Yenye Urefu wa Kilomita 221.5
Mbunge Filikunjombe Amesema Kuwa Kutokana na Wananchi Wengi Kuonekana Kukosa Imani na Wakandarasi Wa Kizalendo Kutokana na Kazi Zao Zilizonyingi Kufanyika Kwa Mashaka,Hivyo Amewataka Wakandarasi Hao Kutumia Fursa Hiyo Kuudhihirishia Umma Kuwa Wanauwezo Mzuri wa Kufanya Kazi Katika Barabara Hizo.
Amesema Kwa Mabaya na Mazuri Watakayoyafanya Katika Barabara Hizo Atakwenda Kupaza Sauti Yake Ya Kuwapongeza Ama Kuwakandamizi Pindi Watakapofanya Vizuri Au Vibaya.
Akitoa Taarifa ya Ukarabati wa Barabara Hizo Utakaofanyika Kwa Muda wa Siku 60 Tangu Kusainiwa Kwa Mikata Hiyo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Toka Wizara ya Ujenzi Mhandisi Patric Mfugale Amesema Kuwa Hadi  sasa Serikali Imeshaingia Mkataba na Mhandisi Mshauri Tangu Februari 20 Mwaka Huu Kwa ajili ya Kufanya Upembuzi Yakinifu,Usanifu wa Kina na Uandaaji wa Makablasha Katika Barabara Hizo Kwa Gharama Ya Zaidi Ya Shilingi Bilioni Moja.
Mhandisi Mfugale Amesema Kuwa Mikataba Hiyo Iliyosainiwa Rasmi  na Wakandarasi Wanne Tofauti Inagharimu Kiasi Cha Shilingi Bilioni Saba na Milioni 846,430,000/=
Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Katika Tukio Hilo Muhimu la Kiuchumi Katika Mkoa wa Njombe na Taifa Kwa Ujumla Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi  Amewataka Wakandarasi Hao Kuhakikisha Wanafanya Kazi Yenye Ubora Mkubwa Kwani Barabara Hizo Licha Ya Kutegemewa Kupitisha Mitambo Itakayofanya Kazi Ya Kuchimba Madini Hayo Lakini Pia  Barabara Hizo Zinategemewa Sana Kupitisha Mazao Ya Kibiashara Mkoani Hapa.
Wakizungumza Mara Baada ya Kusaini Mikataba Hiyo Baadhi Ya Wakandarasi Hao Wamesema Wamejipanga Vizuri Kujenga Barabara Hizo Licha Ya Serikali Kuwapa Muda Mfupi Katika Kufanya Kazi Hiyo.
Zoezi la Kusaini Mikataba Hiyo Muhimu ya Ukarabati wa Barabara Hizo Zenye Urefu wa Takribani Kilomita Mia Mbili ni Moja ya Hatua Kubwa Ya Kuwahakikishia Watanzania Kuanza Rasmi Kwa Zoezi la Uchimbaji Madini Hayo Katika Kukuza Pato La Taifa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top