Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTUMISHI WA IDARA YA AFYA KAHAMA AKUTWA AFIA GESTI


 
Marehemu Munuo akiwa katika gesti hiyo alikokuwa amelala
Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo

Mtumishi wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa Kahama, Mkoani Shinyanga, Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya kulala wageni mjini Kahama.

Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Taarifa zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya saa 6 mchana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.

Jesh la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na kumkuta marehemu Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu nne za mkononi.

Mwili wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.
Marehemu Munuo akiwa katika gesti hiyo alikokuwa amelala
mwili wa Marehemu Munuo baada ya kugeuzwa na kukaguliwa

Mwili wa Marehemu Munuoukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top