Habari
kutoka kata ya Mutukula wilaya ya Missenyi mkoani Kagera nchini
Tanzania zinaarifu kuwa kuna ugonjwa wa ajabu ulioanzia nchini Uganda na
kuua watu wengi.
Imeelezwa
kuwa mtu hujikuta ana mhuri wa namba katika mwili wake na hufariki
dunia baada ya siku za namba hiyo ya mhuri iliyopo katika mwili wake
ambayo hupigwa bila kujijua.
Tayari
leo 13.05.2014 katika kitongoji cha Nyakera kata ya Mutukula wilayani
Missenyi mtoto mwenye umri wa miaka minne (4) amefariki dunia baada ya kupigwa mhuri wa namba 3 juzi mgongoni.
Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanari mstaafu Issa Njiku alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema hajapata taarifa hizo.
Tayari kuna mtu mwingine eneo hilo ana mhuri wa namba 14 kwenye mwili wake.
Nitaendelea kuwafahamisha kuhusiana na ugonjwa huo kadri ninavyopata taarifa.
Na Hilali Ruhundwa-Kagera
Post a Comment