Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
Mkufunzi wa waamuzi nchini, Omari Kasinde kilichotokea jana (Mei 12
mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mbali
ya kuwa Mkufunzi, Kasinde ambaye anazikwa leo (Mei 13 mwaka huu) mchana
katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam pia alikuwa Makamu Mwenyekiti
wa Kamati iliyopita ya Waamuzi ya TFF iliyokuwa chini ya uenyekiti wa
Kapteni mstaafu Stanley Lugenge.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Kasinde enzi
za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mwamuzi
na baadaye mkufunzi na kiongozi..
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kasinde, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu
Tanzania (FRAT) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
Post a Comment