Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda pamoja na wananchi walioungana nae, wakiangalia
jinsi mto Mlalakuwa ulivyoharibiwa kutokana na mvua zinazoendelea
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (mbele) akiongozana na Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kuvuka Mto Mlalakuwa kuongea na
wananchi waliokuwa ng'ambo ya mto.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiwahimiza kuhama wananchi
wanaoishi pembezoni wa Mto Mlalakuwa kutokana na nyumba yao kubomoka na
maji kama inavyoonekana.
Zoezi la usafi halikujali rangi wala taifa..
Mto Mlalakuwa ukiwa safi mara baada ya zoezi kumalizika.
Post a Comment