Bahati
Muriga mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 akipokea mfano wa hundi
yenye thamani ya Tzshs. Milioni 25 aliyoshinda kwa ajili ya vifaa vya
kilimo. Kutoka kulia ni Babu wa kijiji, Epheta Msiga wa DMB na Mkamiti
Mgawe kutoka Oxfam.
Mshiriki
Boniphace Meng'anyi Nyakena akipokea mfano wa hundi ya Tzshs. Milioni
25 alizoshinda katika msimu huu. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa
Oxfam Jane Foster, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika Yamungu Kuyandabila, Babu wa kijiji, mwakilishi kutoka
Datavision International pamoja na Epheta Msiga ambaye ni afisa mradi wa
Maisha Plus kutoka kampuni ya DMB.
Mkurugenzi
Mtendaji wa DMB ambao pia ni waandaaji wa shindano la Maisha Plus
Masoud Ally (Kipanya) akiwa anatoa Miongozo mbalimbali wakati wa Sherehe
hizo za kumpata mshindi wa Maisha Plus Na mama Shujaa wa Chakula 2014
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa Hotuba yake wakati wa
Fainali za kumpata mshindi wa Maisha Plus na Mama shujaa wa Chakula 2014
Mgeni Rasmi katika Fainali za kumpata Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus 2014 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kuyandabila akitoa hotuba yake.
Post a Comment