baada ya ajali hiyo, |
Inavyoonekana kwa nyuma |
hii ni sehemu ya mbele ya gari hilo |
Scania lililogongwa kwa nyuma |
Sehemu ambayo gari hilo dogo liliingia |
AJALI
mbaya iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba
T368 CVK na roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea
usiku wa juzi katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika
mji wa Mafinga.
Taarifa
za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado
halijapatikana alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia nyuma ya
roli hilo lililokuwa limepaki kandakando ya barabara ya Mafinga Dar es
Salaam, akiwa katika mwendo mkali.
Mwanafunzi
wa kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo
amenusurika kufa; binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana
amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa
vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika mkono.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 usiku. Na
baada ya ajali hiyo wasamalia wema waliukumbiza mwili wa marehemu na
majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.
Jeshi
la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa za awali
zinaonesha dereva wa gari hilo alikuwa amelewa wakati akiendesha gari
hilo.
Imechotwa: matukiotz web
Post a Comment