Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwanamke aliyeasi uisilamu akamatwa tena

 


Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema kuwa mwanamke aliyeachiliwa hapo jana kwa kosa la kuasi dini amekamatwa tena.

Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alikuwa amehukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.Watu waliomkata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika kuwa wanajeshi wa serikali.

Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa
                                      chanzo bbc.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top