Askari
wa jeshi la polisi wameshutumiwa kwa kuwajeruhi kwa risasi wanawake
wawili na kumshambulia kwa kipigo kiongozi wa chama cha wananchi CUF
wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Kutokana na
shutuma hiyo dhidi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni,
mwandishi wa ITV amefika katika hospitali ya Mwananyamala walikodaiwa
kufikishwa watu hao watatu na kukutana kwanza na mkurugenzi wa ulinzi wa
chama cha wananchi CUF wilaya ya Kinondoni bwana Mwinyipembe Bakari
akiwa amelazwa huku Bi Zawia Hamisi na Grace Loy walilalamikia kupigwa
risasi wakidaiwa kuondolewa haraka katika hospitali ya Mwanayamala
kutokana na usumbufu wa ujio wa vyombo vya habari,ambapo licha ya
mwandishi kuangaika kwa zaidi ya saa nne kuwatafuta na kuwakuta eneo la
Kisiwani wakihudumiwa na ndugu zao ambapo katika mahojiano wamesema
walikuwa wakisherekea shughuli ya ndugu yao na walijua kuwa sheria
hazuii kufanyika sherehe mchana.
Diwani
wa kata ya Makumbusho bwana Harubu Mohamed amesema wanawake hao
walipigwa risasi huku ndugu zao nao wakija juu wakihoji kwanini askari
walitumia nguvu kubwa kiasi hicho na kushindwa hata kupiga mabomu katika
kutawanya watu hao?
Daktari
aliyehudumia wanawake hao dakta Thomson Minja amesema watu hao
walipigwa na kitu chenye ncha kali na kusababisha matundu yenye kina
kirefu katika baadhi ya sehemu ya miili yao
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kinondoni Camilius Wambura ambaye alikuwa kikazi nje
ya ofisi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kikundi hicho
cha kanga moko moko walikuwa wakifanya mambo ya aibu mbele za watu jambo
ambalo sheria inazuia na kwamba bado uchunguzi unaendelea ili kuweka
wazi kama walipigwa na kitu gani na askari yupi alihusika
on Friday, June 20, 2014
Post a Comment