Baadhi ya wabunge wamelalamikia kutofautiana kwa
taarifa za mapato husani katika sekta ya madini na kutaka kamati ya
madini kukaa pamoja na kamati ya viwanda na biashara kupitia mikataba
yote ya madini na kuishauri serikali kuvunja mikatapa itakayoonekana
haina maslahi kwa taifa.
Wakichangia mjadala wa mwelekeo wa mpango wa
maendeleo pamoja na bajeti ya mwaka 2014/25, baadhi ya wabunge bila ya
kujali itikadi za vyama vyao wamelalamikia takwimu za mapato katika
sekta ya madini kutokuwa za kweli.
Katika mkutano huo wa kumi na tano kikao cha
thelathimni na sita wamesema kitendo vya wizara mablimbali kutofuata
sheria na kukosekana kwa miiko ya uongozi kumechangia ongezeko la
rushwa na ufisadi na kuwa janga kubwa katika taifa na kushangazwa na
taarifa za mapango wa maendeleo wa taifa kutogusia tatizo la rushwa
jambo linaloweza kusababisha mpango huo kutotekelezeka
Post a Comment